Friday, February 19, 2016
Mishkaki Ya Kuku
- Kuku kidari
- Mafuta ya kukaangia
- Vitunguu
- Nyanya
- Pilipili boga
Mchanganyiko wa kuchanganyia mishikaki
Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa
Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa
- Pilipili mbichi iliyosagwa
- Mtindi
- Ndimu
- Chumvi
- Cummin powder au bizari ya pilau)
- Coriander powder au gilgilani)
- Pilipili nyekundu ya unga
- Mdalasini wa unga
- Kata kuku vipande vikubwa kubwa kiasi .
- Changanya kuku na masala ya vitu vyote katika masala ya kurowekea kuku uroweke kwa muda wa masaa.
- Katakata vitunguu, nyanya, pilipili boga vipande kiasi.
- Tunga vipande vya kuku katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers) huku unatunga baina yake kitunguu, nyanya, pilipili boga.
- Tia mafuta kiasi katika kikaango. Mafuta yasiwe mengi hadi yakafunika kuku.
- Tumia mafuta kidogo kidogo kila unapoepua kabaab za kwanza ikiwa yamekauka, unaongeza mafuta kidogo kama kiasi ya robo kikombe.
- Kaanga kababu za kuku katika moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi kuku awive.
- Chakula tayari kwa kuliwa