Mahitaji
- Tambi
- Mayai
- Nyanya
- Vitunguu
- Karoti
- Hoho
- Mdalasini uliosagwa
- Mafuta ya kupikia
- Maji
Jinsi ya kuandaa na kupika
- Katakata tambi zako kwa urefu unaoutaka kisha ziloweke kwenye maji safi ya baridi hadi zilainike.
- Katakata viungo vyote ( Vitunguu, Nyanya, Hoho, Karoti) kisha weka kwenye sahani safi.
- Gonga Mayai yako yanayotosha idadi ya Tambi na kisha weka kwenye bakuli.
- Weka sufuria jikoni na uweke mafuta hadi yachemke.
- Chukua Tambi zilizolowekwa kwenye maji na uziweke jikoni kwenye mafuta yanayochemka huku ukizigeuza geuza hadi zitapoonyesha dalili ya kuiva.
- Changanya mchanganyiko wa Mdalisi kwenye Tambi.
- Changanya mchanganyiko wa viungo huku ukiendelea kugeuzageuza hadi viungo viive.
- Funika mchanganyiko wako na uuache uive hadi utapohakikisha maji yamekauka.
- Baada ya kujiridhisha kuwa chakula chako kimeiva kiipue .
- Weka Mayai yaliyopasuliwa kwenye chakula chako na ugeuze hadi mayai yatapoiva na mvuke.
- Chakula chako kupi tayari kwa kuliwa.
Maelezo zaidi
Chakula hiki kinaweza kuliwa na watu wa rika zote na unaweza kutumia juice katika mlo huu.
0 comments:
Post a Comment