Pages

Monday, February 8, 2016

Wali wa Biriani


Mahitaji 
  • Mchele 
  • Nyama ya ngómbe au kuku
  • Samli 
  • Viazi mbatata 
  • Vitunguu maji 
  • Thomu gram 
  • Tangawizi mbichi 
  • Hiliki 
  • Mdalasini 
  • Mtindi 
  • Siki kiasi
  • Majani ya nanaa
  • Chumvi 
  • Zaafarani kidogo (irowekwe kwa maji ya moto )
  • Tungule ilosagwa
  • Tungule ya kopo

Maandalizi 
  • Menya vitunguu maji uvioshe uvikate, weka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange bila ya kuvivuruga mpaka viwe vyekundu. Vichuje uvitoe halafu vitandaze katika sinia.
  •  Twanga mdalasini na hiliki mpaka viwe laini kama unga. Menya thomu uitwange pamoja na tangawizi mbichi.
  • Kata nyama vipande vikubwa kisha tia chumvi na vitu ulivyovisaga (yaani tangawizi mbichi na thomu) vile vile tia unga unga wa mdalasini na hiliki pamoja na mtindi wa maji. Pika mpaka karibu nyama kuiva kabisa ndipo utie viazi mbatata. Ukiona viazi mbatata zimeshaiva tia siki.Usiache kukauka kabisa, bakiza rojorojo. Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia mchele. Acha utokote, angalia kiini cha wali ukiona umeshaiva uchuje.
  • Angalia sufuria ya nyama na rojo lake lisiwe limekauka kabisa, lazima ziwe na maji kidogo. Chukua vile vitunguu ulivyovikaanga vikapoa uvinyunyuzie juu ya masalo yote (usikoroge). Halafu utie mchele uliouchuja, nyunyuzia maji ya zaafarani juu ya wali wote halafu unyunyuzie samli ile uliyochuja kutoka kwenye vitunguu ulivyovikaanga ienee juu ya wali wote. Kisha funika upalie makaa.
  • Biriani  tayari kwa kuliwa. 
Mambo ya kuzingatia 
Unapotaka kupakua lazima kwanza uutoe wali wote mweupe uutie katika chombo kingine, kisha ukoroge masalo yachanganyike sawasawa kisha ndio uyatie juu ya wali katika kila sahani.

0 comments:

Post a Comment