Pages

Sunday, March 6, 2016

Home Made Ice Cream (made in a blender!)


Friday, February 19, 2016

Juice Mchanganyiko wa Karoti, Tangawizi na ndimu


Mishkaki Ya Kuku

Mahitaji
  • Kuku kidari
  • Mafuta ya kukaangia                                         
  • Vitunguu                                                              
  • Nyanya                                                               
  • Pilipili boga                                                     

Mchanganyiko wa kuchanganyia mishikaki 
Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa   
  • Pilipili mbichi iliyosagwa                                         
  • Mtindi                                                                
  • Ndimu                                                                
  • Chumvi                                                                 
  • Cummin powder  au bizari ya pilau)                
  • Coriander powder au gilgilani)                        
  • Pilipili nyekundu ya unga                                        
  • Mdalasini wa unga                                              
Jinsi ya kuandaa chakula
  • Kata kuku vipande vikubwa kubwa kiasi .
  • Changanya kuku na masala ya vitu vyote katika masala ya kurowekea kuku uroweke kwa muda wa masaa.
  •  Katakata vitunguu, nyanya, pilipili boga vipande kiasi.
  • Tunga vipande vya kuku katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers) huku unatunga baina yake kitunguu, nyanya, pilipili boga.
  • Tia mafuta kiasi katika kikaango. Mafuta yasiwe mengi hadi yakafunika kuku.
  • Tumia mafuta kidogo kidogo kila unapoepua kabaab za kwanza ikiwa yamekauka, unaongeza mafuta kidogo kama kiasi ya robo kikombe.
  • Kaanga kababu za kuku katika moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi kuku awive.
  • Chakula tayari kwa kuliwa

Monday, February 8, 2016

Jifunze kutengeneza PIZZA


Piza hii ni ya mboga mboga na cheese

Mahitaji

1 kilo unga wa ngano

240 gram maji ya vugu vugu

2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula

2 Asali kijiko kidogo cha chai

1 chumvi kijiko kidogo cha chai

1 Amira ya chenga kijiko kidogo cha

Jinsi ya kutengeneza
  • Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
  • Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
  • Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
  • Kama unataka kutumia kesho funika vizuri na weka katika friji. Kama unatumia leo fata maelezo katika picha hapo chini.
Huu ndio muonekano wa mchanganyiko wako wa unga tayari kwa kuandaa kitako cha piza

Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara

Muonekano wa umbo la duara

Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza kama inavyoonekana katika picha usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.

Huu ni mkato wa mboga mbichi nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya kwajili ya piza yako

Baada ya kuweka mchuzi wa nyanya weka juu mboga aina zote kwa mpangilio kama inavyoonekana katika picha

Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka tumia kwaruzo la karoti linafaa

kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese mwagia juu ya hizo mboga kama inavyoonekana katika picha

Sasa piza yako ipo tayari kuchomwa weka kwenye sahani ya bati ili isaidie kuiva upande wa chini pia  oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 - 450 F choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa

Huu ndio muonekano wa piza yako baada ya kuiva unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga  tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.

Na Activechef - Issa Kesu

Jinsi ya Kutengeneza Ice cream nyumbani


Tengeneza Icecream nyumbani bila mashine na kwa muda mfupi

Jinsi ya kutengeneza Juice ya Tikiti maji (Watermelon)

Jifunze kutengeneza Juice ya Tikiti maji ukiwa nyumbani 

Wali wa Biriani


Mahitaji 
  • Mchele 
  • Nyama ya ngómbe au kuku
  • Samli 
  • Viazi mbatata 
  • Vitunguu maji 
  • Thomu gram 
  • Tangawizi mbichi 
  • Hiliki 
  • Mdalasini 
  • Mtindi 
  • Siki kiasi
  • Majani ya nanaa
  • Chumvi 
  • Zaafarani kidogo (irowekwe kwa maji ya moto )
  • Tungule ilosagwa
  • Tungule ya kopo

Maandalizi 
  • Menya vitunguu maji uvioshe uvikate, weka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange bila ya kuvivuruga mpaka viwe vyekundu. Vichuje uvitoe halafu vitandaze katika sinia.
  •  Twanga mdalasini na hiliki mpaka viwe laini kama unga. Menya thomu uitwange pamoja na tangawizi mbichi.
  • Kata nyama vipande vikubwa kisha tia chumvi na vitu ulivyovisaga (yaani tangawizi mbichi na thomu) vile vile tia unga unga wa mdalasini na hiliki pamoja na mtindi wa maji. Pika mpaka karibu nyama kuiva kabisa ndipo utie viazi mbatata. Ukiona viazi mbatata zimeshaiva tia siki.Usiache kukauka kabisa, bakiza rojorojo. Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia mchele. Acha utokote, angalia kiini cha wali ukiona umeshaiva uchuje.
  • Angalia sufuria ya nyama na rojo lake lisiwe limekauka kabisa, lazima ziwe na maji kidogo. Chukua vile vitunguu ulivyovikaanga vikapoa uvinyunyuzie juu ya masalo yote (usikoroge). Halafu utie mchele uliouchuja, nyunyuzia maji ya zaafarani juu ya wali wote halafu unyunyuzie samli ile uliyochuja kutoka kwenye vitunguu ulivyovikaanga ienee juu ya wali wote. Kisha funika upalie makaa.
  • Biriani  tayari kwa kuliwa. 
Mambo ya kuzingatia 
Unapotaka kupakua lazima kwanza uutoe wali wote mweupe uutie katika chombo kingine, kisha ukoroge masalo yachanganyike sawasawa kisha ndio uyatie juu ya wali katika kila sahani.

Mapishi ya Jamii ya Tambi na Mayai


Mahitaji
  • Tambi
  • Mayai
  • Nyanya
  • Vitunguu
  • Karoti
  • Hoho
  • Mdalasini uliosagwa
  • Mafuta ya kupikia 
  • Maji


Jinsi ya kuandaa na kupika
  • Katakata tambi zako kwa urefu unaoutaka kisha ziloweke kwenye maji safi ya baridi hadi zilainike.
  • Katakata viungo vyote  ( Vitunguu, Nyanya, Hoho, Karoti) kisha weka kwenye sahani safi.
  • Gonga Mayai yako yanayotosha idadi ya Tambi na kisha weka kwenye bakuli.
  • Weka sufuria jikoni na uweke mafuta hadi yachemke.
  • Chukua Tambi zilizolowekwa kwenye maji na uziweke jikoni kwenye mafuta yanayochemka huku ukizigeuza geuza hadi zitapoonyesha dalili ya kuiva.
  • Changanya mchanganyiko wa Mdalisi kwenye Tambi.
  • Changanya mchanganyiko wa viungo huku ukiendelea kugeuzageuza hadi viungo viive.
  • Funika mchanganyiko wako na uuache uive  hadi utapohakikisha maji yamekauka.
  • Baada ya kujiridhisha kuwa chakula chako kimeiva kiipue .
  • Weka Mayai yaliyopasuliwa kwenye chakula chako na ugeuze hadi mayai yatapoiva na mvuke.
  • Chakula chako kupi tayari kwa kuliwa.


Maelezo zaidi
Chakula hiki kinaweza kuliwa na watu wa rika zote na unaweza kutumia juice katika mlo huu.