Pages

Monday, February 8, 2016

Jifunze kutengeneza PIZZA


Piza hii ni ya mboga mboga na cheese

Mahitaji

1 kilo unga wa ngano

240 gram maji ya vugu vugu

2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula

2 Asali kijiko kidogo cha chai

1 chumvi kijiko kidogo cha chai

1 Amira ya chenga kijiko kidogo cha

Jinsi ya kutengeneza
  • Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
  • Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
  • Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
  • Kama unataka kutumia kesho funika vizuri na weka katika friji. Kama unatumia leo fata maelezo katika picha hapo chini.
Huu ndio muonekano wa mchanganyiko wako wa unga tayari kwa kuandaa kitako cha piza

Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara

Muonekano wa umbo la duara

Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza kama inavyoonekana katika picha usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.

Huu ni mkato wa mboga mbichi nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya kwajili ya piza yako

Baada ya kuweka mchuzi wa nyanya weka juu mboga aina zote kwa mpangilio kama inavyoonekana katika picha

Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka tumia kwaruzo la karoti linafaa

kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese mwagia juu ya hizo mboga kama inavyoonekana katika picha

Sasa piza yako ipo tayari kuchomwa weka kwenye sahani ya bati ili isaidie kuiva upande wa chini pia  oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 - 450 F choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa

Huu ndio muonekano wa piza yako baada ya kuiva unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga  tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.

Na Activechef - Issa Kesu

1 comment: